Thursday, November 26, 2009
Wanandoa wa–gate crash mnuso wa Obama
Enzi zile bwana, minuso ilikuwa inafuatiliwa kwa nguvu zote, iwe umealikwa au hujaalikwa. Ni bora u–gate crash lakini uwe ndani ya nyumba kuliko kuona aibu ukakosa mnuso wa nguvu. Lakini enzi hizo ilikuwa ni minuso ya majumbani.
Marekani yamezuka ma–gate crashers ya aina yake, yamegaye crash mnuso wa Ikulu. Hawa ni wanandoa wawili kutoka Virginia, Michaele na Tareq Salashi ambao Jumanne walifanikiwa kujipenyeza hadi dhifa ya taifa wakati Barack Obama alipomuandalia waziri mkuu wa India chakula cha jioni.
Msemaji wa Ikulu ameeleza kuwa pamoja na wanandoa hao kumudu ku–gate crash mnuso huo, usalama wa Obama haukutikiswa kwa kuwa taratibu zote za ukaguzi wa mlangoni zilifanyika ingawa Salashi na mkewe walipita hapo hapo bila ya kadi.