Tuesday, January 15, 2008

 

Kakobe umtoa mpya, lakini hakuweka bayana

Katika moja ya kauli ambazo zimeshangaza wengi tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais na wabunge nchini Kenya. Ni kweli kuwa wana harakati wote wangependa kusikia kuwa mtu yeyote aliye katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati analaani matokeo hayo kuwa Bwana Mwai Kibaki ameiba kura.
Lakini Askofu Kakobe aliibuka na jipya aliposema kuwa anampongeza Kibaki kwa kumshinda Raila Odinga. Ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na kumshauri Rais Jakaya Kikwete kutangaza kuitambua serikali ya Kibaki mapema na pia kuwalaumu Watanzania kuwa ni watu wasio wa kweli kwa kushindwa kusema ukweli kuhusu hisia zao.
Lakini Askofu Kakobe hakueleza bayana nini hasa kimemsukuma kutangaza kumuunga mkono Kibaki na kile ambacho pengine anaona kuwa kimemzuia Kikwete kutangaza kumuunga mkono.
Wakati wa mchakato wa kuelekea uchaguzi wa Kenya, Odinga alifanya kosa moja kubwa ambalo ni rafu katika siasa, kuingia katika makubaliano na dini moja na kuacha nyingine zikiwa hazijui mustakabali wao baada ya Odinga kuingia madarakani.
Aliingia makubaliano na Waislamu, na ingawa hatujui kwa undani makubaliano hayo yalikuwa katika maeneo gani, kilichojitokeza dhahiri ni Wakenya waliokimbilia kanisani kuchomwa moto wakiwa hai.
Hadi leo Odinga hajazungumzia hilo na Askofu Kakobe kama kiongozi wa roho za waumini wa Kikristo asingeweza kumuunga mkono mtu aliyeingia makubaliano hayo ambayo baada ya matokeo hayo ya kushangaza kundi la Wakristo wapatao 40 kuchomwa moto wakiwa hai.
Hapa tueleweje?
Ni lazima Askofu Kakobe ampongeze Kibaki!

This page is powered by Blogger. Isn't yours?